Watu
25 wameuawa mjini Mogadishu nchini Somalia baada ya kundi la kigaidi
la Al Shabab kutekeleza shambulizi la bomu katika hoteli maarufu
mjini humo.
Walioshuhudia
milipuko hiyo ya bomu wanasema, baada ya milipuko hiyo miwili,
kulifuatiwa na ufwatulinianaji wa risasi katika hoteli hiyo maarufu
ambayo pia inaelezwa ilikuwa na Mawaziri wa serikali.
Haya
ndio mashambulizi mbaya kuwahi kutokea katika siku za hivi karibuni
mjini Mogadushu katika nchi hiyo inayoendelea kupambana na kundi la
Al Shabab linaloshrikiana kwa karibu na Al Qeada.
Ripoti
kutoka katoka Ikulu ya Mogadishu imethibitsiha maafisa yaliyotokea
baada ya mashambulizi hayo na kusabisha zaidi ya watu 70 kujeruhiwa.
Kundi
la Al Shababa limethibitisha kuhusika na shambulizi la leo na
limekuwa likijaribu kuipundua serikali Hassan Sheikh Mohamud
inayotambuliwa Kimataifa.
Al
Shabab imekuwa ikilenga kutekeleza mashambulizi yake katika Hoteli
mbalimbali, Uwanja wa ndege na Ikulu ya Mogadishu bila mafanaikio.
Maelfu
ya wanajeshi wa Umoja wa Afrika wapo nchini humo kukabilianana kundi
hilo la kigaidi.
Aucun commentaire:
Enregistrer un commentaire