Siku
chache zikiwa zimesalia kabla ya wananchi wa Nigeria kufanya uchaguzi
mkuu wa rais, hii leo nchi hiyo imeendelea kushuhudia mashambulizi
mapya ya kundi la Boko Haram katika mji wa Maiduguri wakati huu
vikosi vya Chad na Cameroon vikiungana na majeshi ya Nigeria
kuwakabili wapiganaji hao.
Mwishoni
mwa juma miji ya Borno na Maiduguri imeshuhudia mapigano makali kati
ya wapiganaji wa Boko Haram na wanajeshi wa Serikali, ambapo majeshi
ya serikali kwa kusaidiwa na raia walifanikiwa kudhibiti miji hiyo na
kuwazuia wapiganaji hao kuichukua tena.
Wakati
majeshi ya Chad na Cameroon yamefanya mashambulizi ya anga kwenye
miji ya Gamboru na mashariki mwa mji wa Borno ambako wapiganaji hao
wameelezwa kujipanga upya.
Kushuhudiwa
kwa mapigano zaidi kati ya vikosi vya Serikali na wapiganaji hawa wa
kiislamu, kumeendelea kutishia usalama wa nchi jirani pamoja na
uchaguzi mkuu unaotarajiwa kufanyika February 14 mwaka huu.
Aucun commentaire:
Enregistrer un commentaire