Shuguhuli
za uzinduzi wa bunge jipya nchini Libya zimeitishwa kufanyika
jumatatu hii katika miji wa Tobrouk na upande wa chama cha wazalendo
na tripoli na chama cha waislam wakati huu mauaji yakiendelea huku
wageni na raia wa kawaida wakiendelea kuikimbia nchi hiyo kutokana na
mapigano
katika mji mkuu
Tripoli mapigano yaliozuka tangu Julay 13 yanaendelea kushuhudiwa
huku watu 22 wakipoteza maisha na wengine 72 wakijeruhiwa katika
mapigano ya mwishoni mwa juma baina ya makundi hasimu.
Takwimu
zinaonyesha kuwa watu 124 ndiuo ambao wameuawa hadi sasa huku wengine
zaidi ya mia tano wakijeruhiwa tangu kuanza kwa mapigano Julay 13
mjini Tripoli. Duru za kitabibu zimearifu kuwa huenda idadi ya
waliopoteza maisha na kujeruhiwa ikawa kubwa zaidi kwani taarifa ya
serikali haizingatii watu waliouawa na kujeruhiwa katika viunga vya
jiji la Tripoli hususan katika mji wa Misrata.
Aucun commentaire:
Enregistrer un commentaire