Rais
wa Marekani Barack Obama amepongeza jana hatuwa ya kuteuliwa kwa
aliyekuwa naibu spika wa bunge Haidar al Abadin kuwa waziri mkuu mpya
nchini Iraq katika hotuba yake ambayo ililenga pia kutowa ujumbe kwa
waziri mkuu alieondolewa madarakani licha ya kutomtaja moja kwa moja
na ambaye ameonyesha nia ya kutoachia madaraka.
Akizungumza
akiwa katika kisiwa cha Martha's Vineyard katika jimbo la
Massachusetts kaskazini mashariki ambako yupo likizo na familia yake,
Obama amefahamisha kwamba ameahidi uungwaji wake mkono kwa waziri
mkuu mpya Haïdar al-Abadin na amewatolea wito viongozi wote wa
kisiasa nchini Irak kufanyakazi kwa mshikamano.
Rais
Obama amesisitiza kuhusu hatuwa ya kuunda baraza la mawaziri hara
iwezekanavyo itayo shirikisha pande zote kwa manufaa ya wananchi wote
wa irak na ambayo itapambana na kundi la wapiganaji wa kiislam la
Isil.
Hapo
jana waziri mkuu wa zamani Nuri Al Malik ambaye utawala wake umekuwa
ukikosolewa vikali na Marekani tangu kipindi kadhaa, amemtuhumu rais
wa nchi hiyo kwa kuvunja katiba baada ya kuchukuwa hatuwa ya kumteuwa
waziri mkuu mpya wakati muhula wake bado haujatamatika.
Aucun commentaire:
Enregistrer un commentaire