Serikali
ya Rwanda imetangaza jana kwamba mtu mmoja anaeonyesha dalili za
maradhi ya Ebola amewekwa mahali pa pekeake mjini Kigali huku
uchunguzi ukiendelea zaidi kubaini iwapo ni maradhi ya Ebola au ni
homa ya kawaida.
Kulingana
na ujumbe wa waziri wa Afya Agnes Binagwaho kwenye mtandao wake wa
Twitter mtu huyo raia a Ujerumani amwekwa katika eneo la pekeake
kwenye Hospital ya mfalme Faisal ambaye anaonyesha dalili za mardhi
ya Ebola na matokeo yatafahamishwa kwa muda saa 48 zijazo.
Hii
itakuwa ni mara ya kwanza kuwepo kwa mshukiwa wa kwanza wa maradhi ya
Ebola nchini Rwanda, maradhi yanayo sumbuwa na kutikisa nchi za
Afrika Magharibi tangu mwanzoni mwa mwaka.
Mwanafunzi
huyo raia wa Ujerumani alikuwa nchini Liberia kabla ya kuwasili
nchini Rwanda.
Aucun commentaire:
Enregistrer un commentaire