Wizara
ya sheria nchini Burundi imesema kwamba Hussein Radjabu kinara zamani
wa chama tawala cha CNDD-FDD hakutekwa bali ametoroka jela kuu la
mpimba na kutokomea katika maeneo yasiojulikana bado.
Kulingana
na naibi msemaji wa wizara hiyo Bigirimana Eliason amesema Hussein
Radjabu ametoroka katika jela kuu la Mpimba katika Usiku wa Jumapili
kuamkia Jumatatu March 2 mwaka 2015 akiwa na wafungwa wengine 4,
pamoja na askari polisi watatu
Naibu
mseji huyo ameeleza kuwa mbali na Hussein Radjabu mfungwa mwingine
Ribakare Baudoin maharufu Ndindi, Ndikuma Remy aliekuwa anahusika na
Ulinzi wake na Irankunda Sirique liaekuwa mpishi pamoja na polisi
watatu.
Hayo
yanajiri wakati huu wakili wa Hussein Radjabu Prosper Niyoyankana
akitishia kufunguwa mashtaka kutokana na mteja wake huyo ambae
haijulikani alipo. Wakili huyo amesema mteja wake amekuwa akifanyiwa
madhila na vitisho vya kuuawa alipokua jela.
Aucun commentaire:
Enregistrer un commentaire