Umoja wa Ulaya kupitia muakilishi wake jijini Bujumbura Patrick Spirlet ameonya kuhusu muhula wa 3 wa rais Nkurunziza katika uchaguzi mkuu wa Rais wa Juni nchini humo kwamba unaweza kuzua machafuko katika nchi hiyo.
Joto
la kisiasa kuelekea kwenye uchaguzi mkuu wa rais nchini Burundi
limeanza kupanda wakati huu kukiwa na shaka kwamba rais Nkurunziza
anampango wa kuwania muhula wa 3, jambo ambalo upinzani unasema ni
kinyume na katiba ya Burundi na makubalinao ya amani ya Arusha.
Hata hivyo chama tawala cha CNDD-FDD kinaona kwamba rais Nkurunziza bado ana nafasi ya kuwania kutokana na muhula wa kwanza kuelezwa kwamba hakuchaguliwa na wananchi bali aliteuliwa kupitia bunge.
Patrick
Spirlet amesema kumekuwa na maoni tofauti kuhusu muhula huu wa 3,
hivyo wametaka maoni hayo yasikilizwe wakati huu tayari kanisa
katoliki na Mashirika ya kiraia yameonyesha kupinga hatuwa hiyo
ambayo hata hivyo Nkurunziza hajatangaza bayana kwamba atawania
muhula mwingine.
Jumuiya ya kimataifa inatiwa wasiwasi na hali ya kisiasa nchini Burundi kuelekea kwenye uchaguzi mkuu wa rais, lakini hii ni mara ya kwanza kabisa kwa Umoja wa Ulaya kuonyesha msimamo wake kuhusu muhula wa 3 wa rais Nkurunziza.
Patrick Spirlet amesema amani nchini Burundi bado ni legelege hivyo inabidi kuheshimu katiba ya nchi hiyo na kuheshimu pia mkataba wa amani wa Arusha uliofikia kusitishwa kwa vita mwaka 1993-2006
Akijibu
hoja hii ya Umoja wa Ulaya waziri wa mambo ya nje wa Burundi Laurent
Kavakure amesema mkataba wa Arusha sio bibilia ambayo haiwezi
kubadilishwa.
Aucun commentaire:
Enregistrer un commentaire