wakati
kampeni ya kupiga vita mauaji ya watu wenye umelavu ikiendelea nchini
Tanzania, polisi nchini humoe imsesma hapo jana kwamba mtoto mmoja
mwenye ulemavu wa ngozi amekatwa Kiganja cha mkono wake wa kushoto na
kundi la watu wasiojulikana.
Baraka
Cosmos mtoto mwenye ulemavu wa ngozi alikuwa amelala na mama yake
katika kijiji cha Kipenda kusini magharibi mwa Mkoa wa Rukwa ambapo
kundi la majambazi waliingia na kumteka mtoto huoyo kabla ya
kumjeruhi mama yake.
Duru
za polisi zinaeleza kwamba majambazi hao walimpiga mama wa mtoto huyo
Prisca Shabani baada ya kukataa kuwapa mwanae na ambapo walitumia
panga kwa kukata kiganja cha mkono wa kushoto wa mtoto huyo ambae
baadae alipelekwa Hospitalini na mama yake.
Juma
lililopita mahakama kaskazini mashariki mwa Tanzania iliwahukumu
kunyongwa watu wanne kwa kuhusika na mauji ya mwanamama mmoja mlemavu
wa ngozi.
Tukio hili linatokea wakati huu nchini Tanzania kukwa na kampeni kambambe ya kupiga vita mauaji ya watu wenye ulemavu wa ngozo (Albino)
hii ni ishara kwamba kampeni hiyo imefeli, na watu waache kuuza sura kwenye mitandao ya kijamii kwa kuendesha shughuli zisizokuwa na matunda mazuri.
Aucun commentaire:
Enregistrer un commentaire