Watu
zaidi ya 20 wamejeruhiwa wawili wakiwa katikahali mbaya wakiwa ndani
ya ndege bada ya ndege hiyo kupata hitilafu ambapo ilikuwa ikitokea
nchini Afrika Kusini kuelekea mjini Hong Kong nchini China
Majeruhi
walisafirishwa haraka sana Hospitalini baada tu ya ndege hiyo ya
south African Airlines kutuwa ambapo ilikuwa na jumla ya habiria 165.
Taarifa
kutoka kampuni hiyo zinasema watu 25 ndio walijeruhiwa wakiwemo
wafanyakazi wa ndani ya ndege. Hata hivo hakuna sababu zozote
zilizotolewa na kampuni hiyo katika taarifa hiyo.
Msemaji
wa mamlaka ya anga jijini hong Kong amesema kulikuwa na hali ya
hatari iliotokea wakati ndege hiyo ikiwa katika anga la malaysia.
Habiria
walionusurika wamesema kulitokea na mtikisiko uliodumu dakika kadhaa
ambapo habiria waligonga vichwa kwenye paa, rubani wa ndege hiyo
aliomba msaada wa matibabu kwa habari waliokuwa ndani ya ndege hiyo
wakati tu akijiandaa kutuwa kwenye uwanja wa ndege wa Hong Kong.
Aucun commentaire:
Enregistrer un commentaire