Siku
nne zikiwa zimesalia kabla ya siku ya saba saba kuwadia nchini Kenya
ambapo muungano wa upinzani, CORD, umepanga kufanya mkutano mkubwa
kushinikiza kufanyika kwa mazungumzo ya kitaifa, kamati maalumu ya
bunge la kitaifa na Seneti imeundwa kujaribu kunusuru mvutano kati ya
CORD na Jubilee.
Kamati
hiyo inayojumuisha wajumbe 33 toka kila upande unaohusika kwenye
mzozo huo, itaongozwa na mwenyekiti ambaye hatoki upande wowote wa
kisiasa unaovutana kuhusu kufanyika ama kutofanyika kwa mazungumzo ya
kitaifa.
Mutava
Musyimi ni mbunge wa Mberee Kusini nchini Kenya na yeye ndiye
aliyehusika kwa sehemu kubwa kuandaa na kuundwa kwa kamati hii
maalumu ya wabunge.
Licha
ya kamati huu kutangazwa kuundwa na kuwahusisha wabunge toka pande
zote mbili, kiongozi wa muungano wa JUBILEE kwenye bunge la kitaifa
Aden Duale ameendelea kusisitiza muungano wao kutojihusisha na
mazungumzo haya kamwe.
Katika
hatua nyingine muungano wa CORD umesisitiza kufanyika kwa mkutano wao
siku ya Jumatatu na kwamba polisi imeruhusu mkutano wao kufanyika na
kuahidiwa usalama.
Kinara
wa muungano wa CORD Raila Odinga na wenzake wanashinikiza musuala
muhimu matano kujadiliwa kati yake na rais Uhuru Kenyatta pamoja na
naibu wake William Ruto.
Aucun commentaire:
Enregistrer un commentaire