Zaidi
ya wanajeshi 500 wa Marekani waliotumwa nchini Iraq kulinda ubalozi
wake wameelezwa kuwa watakuwa na uwezo wa kutumia ndege za kivita
pamoja na zile zisizo na rubani kwaajili ya usalama mjini Baghdadi,
Pentagon imesema.
Jumatatu
ya wiki hii rais Barack Obama aliagiza kuongezwa kwa wanajeshi 200
zaidi nchini Iraq kuhakikisha maofisa wake wa Ubalozi wanakuwa salama
wakati huu vikosi vya Serikali ya Iraq vikiendelea kukabiliwa na
upinzani toka kwa waasi wa kiislamu wa ISIL.
Jeshi
la Iraq limezidisha mashambulizi kwenye mji wa Tikrit alikozaliwa
marehemu Saddam Hussein, mji ambao unakaliwa na wapiganaji hao ambao
wametangaza utawala wa kiislamu.
Aucun commentaire:
Enregistrer un commentaire