Nchi
za Jumuiya ya ukanda wa maziwa makuu ICGLR zimewapa muda wa ziada
waasi wa kihutu kutoka Rwanda waliopiga kambi nchini DRCongo
kujisalimisha kwa khiari ili kuepusha mashambulizi ya kijeshi dhidi
yao kwa kipindi cha miezi sita kuanzia sasa.
Kwa
mujibu wa taarifa ya pamoja ya mawaziri kutoka nchi wanachama wa
ICGLR pamoja na wale wa Jumuiya kiuchumi ya nchi za Kusini mwa Afrika
SADC, wajumbe hao wamepokea uamuzi wa kundi la FDLR kujisalimisha na
silaha zao, hivyo mpango wa kujisalimisha unatakiwa kutekelezwa kwa
kipindi cha miezi sita ijayo kuanzia Julay 2.
Viongozi
hao wamelitahadharisha kundi hilo la FDLR iwapo halitotekeleza hatuwa
hyo kwa muda uliotolewa, basi watakabiliwa na hatuwa ngumu.
Kikao
hicho cha mawaziri wa ICGLR kimetowa wito pia kwa ajili ya
uimarishaji wa utaratibu wa tathmini na utekelezaji wa upunguzaji wa
silaha na kuwarejesha makwao wapiganaji hao nchini Rwanda. Hakuna
ufumbuzi mwingine uliotolewa na hakuna mapendekezo, yaliotolewa na
Monusco pamoja na serikali ya Congo juu ya waasi ambao hawatopendelea
kurejea nchini Rwanda.
Taarifa
hiyo ya pamoja ilitolewa baada ya majadiliano ya muda mrefu hapo jana
jijini Luanda. Wajumbe katika mkutano huo walivutana kuhusu muda
uliotolewa, baadhi ya nchi kama vile Rwanda na Angola zilipendekeza
waasi hao wapewe muda mfupi mathalan miezi mitatu. Lakini mwishowe
wajumbe hao waliafikiana kutowa muda wa miezi sit
Aucun commentaire:
Enregistrer un commentaire