Bernard Membe |
Serikali
ya Tanzania imeendelea kusisitiza kuwa, itashirikiana na nchi
wanachama za Jumuiya ya Afrika Mashariki na nchi za maziwa makuu
katika kusaka suluhu ya mzozo wa Jamhuri ya kidemokrasia ya kongo DRC
na kwamba serikali ya Rwanda izungumze na waasi wa FDLR.
Akizungumza
na wanahabari jijini Dar Es Salaam waziri wa mambo ya kigeni wa
Tanzania Bernard Membe amesema kuwa kwenye mkutano wa Umoja wa Afrika
na ule wa SADC, viongozi wakuu walikubaliana kuwa waasi wa FDLR ni
lazima wajisalimishe na kwamba Serikali ya Rwanda iwajumuishe baadhi
ya wapiganaji hao kwenye jeshi lake.
Kauli
hii inatolewa wakati huu nchi ya Rwanda kupitia kwa rais Paul Kagame
ikisisitiza kutokuwa tayrai kufanya mazungumzo yoyote na waasi wa
FDLR wala kuwajumuisha kwenye serikali yake.
Waziri
Membe anasema ili suluhu ipatikane nchini DRC na jirani yake Rwanda
ni lazima waasi wa FDLR wajisalimishe na Serikali ya Rwanda ikubali
kuwarejesha nchini mwake.
Aucun commentaire:
Enregistrer un commentaire