Wahanga
wa mauaji ya ajali ya moto uliotokana na kuteketea kwa lori la mafuta
katika kijiji cha Sange Mkoa wa Kivu ya Kusini kwenye umbali wa
kilometa takriban 70 na mji wa Biukavu, wamekumbukwa hapo jana. Ajali
hiyo ilitokea miaka minne iliopita Julay 2 mwaka 2010 na kugharimu
maisha ya watu zaidi ya 220.
Lori
hilo la mafuta lilipata ajali katika kijiji hicho, ambapo mafuta
yalivuka, na ndipo wananchi wa eneo hilo wakasogea kwa ajili ya
kuchota mafuta, jamboo ambalo lilikuwa hatari sana kwako.
Baada
ya muda kadhaa, lori hilo lililipuka na kusababisha maafa hayo
makubwa ya wananchi na hata nyumba mali na vitu vilivyokuwa karibu
vyote viliteketea. Rais wa taifa hilo Joseph Kabila siku mbili baada
ya kutokea kwa ajali hiyo mbaya kuwahi kutokea alizuru katika eneo
hilo na kutangaza siku mbili za maombolezo ya kitaifa.
Aucun commentaire:
Enregistrer un commentaire