Kwa
mara ya kwanza serikali ya Marekani imethibitisha kuwa imekuwa na
kikosi maalumu nchini Somalia ambacho kimekuwa kikifanya kazi kwa
siri toka mwaka 2007 licha ya utawala wa nchi hiyo mara kadhaa
kukanusha taarifa hizo.
Kwa
mujibu wa afisa mmoja wa jeshi la Marekani, amesema kuwa nchi yake
inawanajeshi zaidi ya 120 nchini Somalia ambao kazi yao imekuwa ni
kutoa mafunzo na ushauri kwa vikosi vya Serikali.
Taarifa
hii ya Marekani inatolewa wakati huu wanamgambo wa Al-Shabab nchini
Somalia wameapa kuendelea na mashambulizi yao dhidi ya nchi ambazo
zinawanajeshi wake nchini Somalia pamoja na zile zinazotoa mafunzo.
Aucun commentaire:
Enregistrer un commentaire