Umoja
wa Mataifa imeikosoa hatuwa ya serikali ya burundi ya kuendelea
kumuweka korokoroni mkurugenzi wa kituo kimoja cha radio ya kibinafsi
RPA, Bob Rugurika kwa tuhuma za kuhusika katika mauaji ya watawa 3
raia wa italia waliouawa mwishoni mwa mwaka uliopita.
Msemaji
wa kitengo cha haki za binadamu kwenye Umoja huo Ravina Shamdasani
amesema hakuna mtu anaestahili kutiwa jela kutokana tu na kunyimwa
hai yake ya msingi ya kujieleza.
Bob
Rugurika alikamatwa mwezi januari uliopita baada ya kituo chake
kupeperusha sauti ua mtu aliekiri kwamba ndiye aliehusika na wenzake
kutekeleza mauaji huku akiwataja viongozi kadhaa wa serikali ya
Burundi kuwa ndio waliopanga mauaji hayo ya watawa vikongwe kabisa
raia wa Italia.
Mapema
wiki hii mahakama moja nchini Burundi imetupilia mbali ombi
la mawakili wa Bob Rugurika la kuachiwa huru kwa dhamana.
Aucun commentaire:
Enregistrer un commentaire