Rais Obama na Russ Feingold |
Serikali
ya Washington inasisitiza msimamo wake wa kutaka kalenda ya jumla ya
uchaguzi nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo itangazwe na Tume ya
Uchaguzi CENI haraka iwezekanavyo.
Kauli
hiyo ya Marekani imetolewa na Mjumbe maalum wa Rais Obama katika
Ukanda wa Maziwa makuu Russ Feingold katika mukutano na waandishi wa
habari hapo jana mjini Kinshasa.
Hadi
sasa, Tume hiyo imechapisha ratiba ya uchaguzi wa serikali za mitaa,
wa manispaa na miji uliyopangwa kufanyika mwaka huu, lakini Marekani
inaamini kuwa kupitishwa kwa sheria mpya ya uchaguzi kungeweza
kuharakisha kutolewa kwa kalenda hiyo, amesema Russ Feingold.
Aidha,
Fengold amesisitiza kuwa lazima uchaguzi wa rais ufanyike kabla ya
mwisho wa mwaka 2016 ambapo Rais Joseph Kabila anatarajiwa kuachia
ngazi, na kuongeza kuwa nchi yake inatetea makabidhiano ya madaraka
kwa njia ya amani na ya kidemokrasia nchini DRC na barani Afrika.
Kuhusiana
na ucheleweshwaji unaoweza kusababishwa na ukosefu wa fedha katika
uchaguzi huo, Feingold ametangaza msaada wa nchi yake wa dola za
kimarekani milioni 20, na kusisitiza kuwa ukosefu wa fedha hauwezi
kuwa sababu ya kutofanya uchaguzi nchini DRC.
Aucun commentaire:
Enregistrer un commentaire