Viongozi
wa Ukraine, Urusi, ufaransa na Ujerumani wanakutana hii leo jumatano
jijini Minsk katika mkutano unaonekana kuwa bahati ya mwisho ya
kupatikana kwa suluhu ya mzozo wa kivita uliodumu kwa zaidi ya miezi
kumi sasa na kugharimu maisha ya watu 5.300 mashariki mwa Ukraine.
Mengi zaidi na Ali Bilali.
Mkutano
huo unawaleta pamoja Angela Merkel, Francois Hollande, Petro
Poroshenko na Vladimir Poutine ikiwa ni matokeo ya juhudi za Ufaransa
na Ujerumani ambapo mwishioni mwa juma lililopita viongozi wa mataifa
hayo walielekea Kiev na Moscu.
Hayo
yanajiri wakati mapigano ya hapo jana yakigharimu maisha ya watu 37.
rais
Poroshenko alipoingia madarakani aliahidi kumaliza machafuko na
kurejesha kwenye himaya ya serikali miji iliojitenga na ambayo
inakaliwa na waasi wanaodaiwa kuungwa mkono na Urusi. Viongozi katika
mkutano huo wa Minsk nchini Belarusi wanataraji kupata makubaliano ya
kusitisha vita bila masharti yoyote na kuondolewa kwa silaha
nzitonzito kwenye uwanja wa mapigano.
Hapo
jana wapiganai wanaodai mjitengo na Ukraine wamejadiliana kwa saa
kadhaa jijini Minsk na wamjumbe wa kiev wakiwa pamoja na wawakilishi
wa Urusi na wa jeshi la ulinzi wa bara la Ulaya OSCE. Waasi waho
wamewasilisha mapendekezo yao ya kumaliza machafuko mashariki mwa
ukraine.
Hata
hivyo kulingana na muakilishi wa taifa lililojitanga na ukraine la
Donetsk Denis pouchline ambae hakuweka wazi yaliomo katika
mapendekezo hayo amesema bado ni mapema kuzungumzia usitishwaji wa
mapigano.
Upande
wake rais wa marekani Barack obama hapo jana amdwasiliana na rais wa
Urusi Vladimir aPoutine pamoja na rais wa ukrainr Petro Poroshenko.
Taarifa ya Ikulu ya marekani imesema kwamba iwapo Urusi itaendeleza
uvamizi wake nchini Ukraine kwa kuwatuma wanajeshi wake, na silaha na
hata kuwafadhili waasi, basi Athari kwa Urusi zitakuwa kubwa.
Aucun commentaire:
Enregistrer un commentaire