Rais
wa Tanzania Jakaya Mrisho Kikwete amekiri kuwa kukosekana kwa msaada
wa kisheria kwa wale wasio na uwezo wa kulipia huduma ya uwakili ni
kikwazo kwa watu hao kupata fursa ya kupata haki.
Rais
Kikwete ametoa kauli hiyo hii leo katika maadhimisho ya siku ya
sheria yaliyofanyika jijini Dar es Salaam na kuratibiwa na mhimili wa
mahakama na kuongeza kuwa kukosekana kwa msaada wa kisheria ni tatizo
linalowakabili watu wengi.
Rais
Kikwete amesema kuwa Serikali italifanyia kazi pendekezo hilo
lililotolewa Mahakama ili kupanua fursa kwa watu wengi kupata haki
ya kisheria na ikiwezekana serikali igharamie huduma za uwakili kwa
watuhumiwa wasio na uwezo kifedha nje ya watuhumiwa wa makosa ya
mauaji.
Aucun commentaire:
Enregistrer un commentaire