Kongamano
la wadau wa elimu kutoka barani Afrika limefungulia rasmi na rais wa
Kenya Uhuru Kenyatta jijini Nairobi.
Watalaam
kutoka zaidi ya mataifa ya 50 wanakutana kujadili ubora na kiwango
cha elimu barani Afrika na namna elimu inavyoweza kuboreshwa.
Mbali
na maswala ya elimu, wadai hao wanajadili haki kwa watoto kupata
elimu katika mataifa yote ya Afrika na mchango wa serikali kufikia
malengo hayo.
Rais
Kenyatta amewaomba walimu nchini Kenya, kuwa wavumilivu wakati huu
serikali ikijitahidi kuhakikisha kuwa wanafanya kazi katika mazingira
mazuri.
Zaidi
ya walimu elfu 2 wanaofanya kazi katika Kaunti za Mandera, Garisa na
Wajir wamekuwa wakiandamana jijini Nairobi kwa mwezi mmoja sasa
wanakiishiniza serikali kuwaahamisha kutoka maeneo hayo yanayopakana
na nchi ya Somalia kwa hofu ya usalama kutoka kundi la Al Shabab.
Aucun commentaire:
Enregistrer un commentaire