Pages

jeudi 19 février 2015

HALAIKI WAJITOKEZA KUMPOKEA BOB RUGURIKA JIJINI BUJUMBURA



Wakaazi wa jiji la Bujumbura wamefurika kwa wingi katika barabara za jiji hilo kumpokea mkurugenzi wa radio RPA Bob Rugurika ambae ameachihuru kwa dhamana kutoka katika jela la Mkoani Muramvya kwenye umbali wa kilometa zaidi ya 60 na jiji la Bujumbura. Imekuwa vigumu kukadiria idadi kamili ya umati huo uliojitokeza kuimba kucheza na kuonyesha furaha yao.

Hapo jana usiku polisi kutoka jijini bujumbura ilikwenda kumtowa jela mkurugenzi huyo jambo ambalo alipinga katu katu akihofia usalama wake, kwani hakuna taifa lolote duniani linalo amuru mfungwa kutolewa jela Usiku.


Mahakama ya rifaa ya jijini Bujumbura iliamuru kuachiwa huru kwa dhamana kwa muandishi huyo wa habari ambae pia ni mkurugenzi wa radio moja ya kibinafasi inayo sikika zaidi jijini Bujumbura ambae anatuhumiwa kuhusika katika mauaji ya watawa 3 raia wa Italia na kutiwa mbaroni tangu mwezi Januari.

Radio RPA inachukuliwa kuwa karibu zaidi na upinzani ni miongoni mwa radio zinazo sikilizwa kwa asilimia kubwa na wananchi wa Burundi. Kuzuiliwa kwa Bob Rugurika kulikosolewa vikali na wananchi wa Burundi pamoja na upinzani lakini pia mashirika ya kiraia bila kuweka kando jumuiya ya kimataifa na mashirika yanayo tetea haki za binadamu.

Mahakama hiyo inamtuhumu Bob Rugurika kutumia sauti ya mtu ambae alikiri kuhusika katika mauaji ya watawa hao watatu raia wa Italia wenye umri wa miaka 75, 79, 83 waliouawa mwezi Septemba mwaka jana Wilayani Kamenge kaskazini mwa Bujumbura. Mtu huyo anawatuhumu viongozi kadhaa wa serikali akiwemo aliekuwa mkuu wa idara ya upelelezi Adolphe Nshimirimana.

Mahakama ya Bujumbura ilimtia nguvuni mtu mmoja raia wa Kamenge kuwa ndie muhusika wa mauaji hayo. Jambo ambalo raia wa eneo hilo wanasema mtu huyo hawezi kuhusika na mauaji kwani ni mpungufu wa akili wa muda mrefu na watu wote wa eneo hilo wanamfahamu.

Yote haya yanajiri ikiwa ni siku kadhaa kabla ya kuelekea kwenye uchaguzi mkuu wa rais, bunge, tarafa wakati huu joto la kisiasa likionekana kushika kasi katika nchi yenye historia ya mauaji ya kisiasa na kikabila.

Rais wa sasa Pierre Nkurunziza anatuhumiwa kuwa na mpango wa kuwania muhula wa 3, jambo ambali ni kinyume na katiba ya nchi hiyo na kuendelea kuuminya upinzani na kuwanyima haki ya kujieleza.

Aucun commentaire:

Enregistrer un commentaire

KINACHOFANYWA NA RAIS NKURUNZIZA KWA SASA NDIO ULE MCHEZO WA NDANI?

Mkanganyiko umeendelea kushuhudiwa katika chama tawala nchini Burundi cha CNDD-FDD, chama ambacho hapo awali kilileta matumaini ya kuwau...