Raymond Tchibanda na Didier Raynders |
Serikali
ya Ubelgiji imemuomba rais Joseph Kabila wa Jamhuri ya Kidemokrasia
ya Congo kuridhia msaada wa kijeshi wa vikosi vya kimataifa MONUSCO
katika kukabiliana na waasi wa kihutu wa FDLR mashariki mwa nchi
hiyo.
Ombi
hilo limewasilishwa na Naibu Waziri Mkuu mwenye dhamana ya
Ushirikiano na Maendeleo, Dekro Alexander na mwenzake wa Mambo ya
Nje, Didier Reynders walioko ziarani mjini Kinshasa.
Katika
mkutano wao na Waziri Kwa Congo Raymond Tshibanda siku ya Jumapili,
mawaziri hao wamemuomba mwenyeji wao kukubali ushirikiano na msaada
wa MONUSCO katika kuwasaka waasi wa FDLR, huku waziri Tshibanda
akielezea uwezekano huo kwa masharti ya kuheshimu uhuru wa Jamhuri ya
Kidemokrasia ya Congo.
Juma
lililopita, Joseph Kabila aliwaambia mabalozi wa kimataifa mjini
Kinshasa kuwa nchi yake haiitaji tena msaada wa vikosi vya MONUSCO
katika operesheni ya kuwapokonya silaha waasi hao na kukosoa tabia
yao ya kuingilia masuala ya ndani ya nchi yake.
Awali
MONUSCO kwa upande wake wamekataa kutoa msaada wa kijeshi kwa
operesheni hiyo kufwatia uteuzi wa majenerali wawili ambao
wanatuhumiwa kushiriki katika vitendo vya ukiukwaji mkubwa wa haki za
binadamu kuendesha operesheni hiyo.
Aucun commentaire:
Enregistrer un commentaire