Pages

lundi 10 février 2014

MAHAKAMA YA ICC KUAMUWA IWAPO BODCO NTAGANDA ANA KESI YA KUJIBU

Mahakama ya uhalifu ya kivita ya ICC inataraji kusikiliza leo Jumatatu kesi ya mauaji ya kivita inayo mkabili mbabe wa zamani wa kivita nchini DRCongo Bosco Ntaganda aliye julikana kama Terminator kufuatia ukatili wake.

Mahakama hiyo itaamuwa iwapo tuhuma za ubakaji, mauaji na uporaji vilivyotekelezwa mashariki mwa DRCongo. Wananchi wa maeneo hayo wanasubiri kwa hamu na gamu kesi.

Kiongozi wa zamani waasi nchini Congo (DRC) Bosco Ntaganda alijisalimisha machi 17 mwaka 2013 katika ubalozi wa marekani  nchini Rwanda ambako alikimbilia.

Bosco alikuwa akitafutwa na mahakama ya uhalifu wa kivita ICC.

Kwa mara ya kwanza akipandishwa kizimbani kwenye mahakama ya kimataifa ya uhalifu wa kivita ya ICC, jenerali Bosco Ntaganda alisisitiza kuwa hana hatia kuhusu tuhuma zinazomkabili mbele ya mahakama hiyo.

Jenerali Ntaganda anakabiliwa na mashtaka kumi ikiwemo kuamuru Ubakaji, mauaji na kutumia watoto kwenye jeshi lake kufanya uasi mashariki mwa nchi hiyo.

Ntaganda aliyekuwa akifahamika kama "The Terminator" alishirikiana na makundi mengi ya uasi mashariki mwa nchi hiyo licha ya kuwa aliwahi kuwa kiongozi wa juu kwenye jeshi la Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo DRC.

Aucun commentaire:

Enregistrer un commentaire

KINACHOFANYWA NA RAIS NKURUNZIZA KWA SASA NDIO ULE MCHEZO WA NDANI?

Mkanganyiko umeendelea kushuhudiwa katika chama tawala nchini Burundi cha CNDD-FDD, chama ambacho hapo awali kilileta matumaini ya kuwau...