Hatuwa
ya kuchaguliwa kwa Prosper Bazombaza kuwa makam wa kwanza wa rais wa
Jamhuri YA Burundi na bunge la nchi hiyo, huenda ikahatarisha zaidi
mzozo wa kisiasa uliopo nchini humo baina ya utawala wa nchi hiyo na
chama cha UPRONA.
Prosper
Bazombaza ambaye ni mfuasi wa chama Uprona, amechaguliwa jana na
wagunge waliowengi kutoka chama cha CNDD-FDD, jumla ya wabunge 84
waliokuwa bungeni, 82 wamemkubali, huku wabunge wa chama chake ambao
hawakuwa bungeni wamepinga uteuzi wake wakisema kwamba ni hujuma za
chama tawala dhidi ya chama hicho Uprona.
Mzozo
huo wa kisiasa baina ya chama tawala na mshirika wake wa karibu
uliibuka tangu mwishoni mwa mwezi Januari baada ya jaribio la chama
cha CNDD-FDD kumuweka mtu wa karibu wa chama hicho kwenye uongozi wa
chama Uprona, hatuwa iliopingwa na aliyekuwa makam wa rais Bernard
Busokoza ambaye alitumuliwa kwenye uadhifa wake.
Msemaji
wa chama Uprona Bonaventure Gasutwa amesema hizi ni hujuma za chama
tawala dhidi ya chama Uprona, na hii ni hatari sana kwa amani ya
Burundi kwakuwa ni uvunjifu dhahiri wa katiba ya Burundi
Upande
wake msemaji wa rais wa burundi Willy Nyamitwe amesema kulikuwa
umuhimu mkubwa wa kupatikana kwa makam wa rais, hivo chama Uprona
kiliwasilisha wagombea na tayari makam wa rais amepatikana vinginevyo
mkangayiko katika siasa ni jambo la kawaida.
Aucun commentaire:
Enregistrer un commentaire