Takriban
watu saba wamepoteza maisha katika shambulio la kuvizia lililotokea
mjini Mogadishu nchini Somalia ambalo Kundi la Al Shabab limejigamba
kuhusika. Kiongozi wa Polisi Ahmed Mumin amesema idadi hiyo inaweza
kuongezeka kwani kuna waliojeruhiwa na wapo katika haloi mahtuti.
Gari
lililokuwemo vilipuzi lililipuka katika pwani ya Lido karibu na makaa
makuu ya idara ya ujasusi.
Msemaji
wa Al Shabab Abu Musab amesema alshabab ndio walioendesha shambulio
hilo dhidiya maafisa wa usalama na wanaimani kuwa miongoni mwa
maafisa hao wa usalama wamepoteza maisha katika shambulio hilo
Kundi
la Al Shabab lenye mafungamano na kundi la kigaidi la Al Qaeda
limezidisha hujuma dhidi ya vikosi vya usalama tangu kufurushwa
katika jiji la Mogadishu na vikosi vya Umoja wa Afrika Amisom Agosti
mwaka 2011
Aucun commentaire:
Enregistrer un commentaire