Hatimaye
Ikulu ya Mogadishu nchini Somalia imerejea kwenye umiliki wa vikosi
vya Serikali, kufuatia mashambulizi ya makomandoo wa Al-Shabab
waliojaribu kuvamia ikulu ya rais.
Waziri
wa ulinzi wa Somalia, Abdikarim Hussein Guled amewaambia wanahabari
mjini Mogadishu kuwa baada ya saa kadhaa za makabiliano kati ya
vikosi vya Serikali na wanamgambo hao wamefanikiwa kuwafurusha na
kuilinda Ikulu ya rais Hassan Sheikh Mohamud.
Wanamgambo
wa Al-Shabab walitumia magari kujitoa muhanga na kurusha maroketi
kwenye Ikulu lakini hawakufanikiwa kuingia ndani, kufuatia ulinzi
mkali uliopo kwenye Ikulu ua Mogadishu.
Umoja
wa Mataifa UN umesema kuwa rais, Hassan Sheikh Mohamud hakujeruhiwa
kwenye shambulio hilo, ambalo ni kubwa zaidi kuwahi kufanywa na
wanamgambo hao kulenga Ikulu ya Mogadishu.
Aucun commentaire:
Enregistrer un commentaire