Pages

mardi 25 février 2014

THABO MBEKI MSULUHISHI WA MGOGORO WA SUDAN AWASILI JIJINI KHARTOUM



Msuluhishi wa Umoja wa Afrika katika mgogoro wa Sudani rais wa zamani wa Afrika Kisini Thabo Mbeki amewasili jijini Khartoum kwa ajili ya kusaidi kushinikiza mazungumzo ya amani karti ya serikali na waasi wa jimbo la Kordofan kabla ya kuanza kwa mazungumzo jijini Addis Ababa nchini Ethiopia.
Mazungumzo kati ya wajumbe wa serikali ya rais Omar hassan al Bashir na waasi wa jimbo la Kordofan yanatarajiwa siku ya Ijumaa mjini Addis Abeba nchini Ethiopia.
Msuluhishi wa Umoja wa Afrika Thabo Mbeki ambaye ni rais wa zamani wa Afrika Kusini anafanya ziara jijini Karthoum itayofuatiwa na mkutano wa tume ya pande tatu ya kimataifa ilioundwa katika mazungumzo ya amani mwaka 2011 kati ya serikali ya Kharthoum na kundi hasimu la waasi wa Kordofan.
Hayo yanajiri wakati pande hizo mbili husika na mzozo nchini Sudani zinajadili kuhusu pendekezo lililotolewa na msuluhishi wa Umoja wa Afrika juu ya usitishwaji mapigano utaoruhusu mashirika ya misaada kuwafikia mamia ya watu waliokwama katika eneo la machafuko na ambao wanahitaji msaada wa kibinadamu.
Usuluhisi ulitowa pendekezo hilo kwa nyakati tofauti kwa serikali ya Khartoum na waasi wa kundi la SPLM-N baada ya kuahirisha mazungumzo jijini Addis Abeba. Pande hizo mbili zinatuhumiana kutokuwa na nia thabiti ya kumaliza machafuko.
Mazungumzo kati ys Karthoum na waasi yanalenga kusitisha mzozo wa miaka mitatu katika eneo la Kordofan Kusini na Nile Bleu, mzozo uliowagusa watu zaidi ya milioni moja.
Hadi sasa haijulikani takwimu za watu walipoteza maisha katika majimbo ya Kordofan Kusini na Bleu Nile, lakini Umoja wa Mataifa unasema takriban watu milioni moja na nusu wameguswa na mzozo huo.

Aucun commentaire:

Enregistrer un commentaire

KINACHOFANYWA NA RAIS NKURUNZIZA KWA SASA NDIO ULE MCHEZO WA NDANI?

Mkanganyiko umeendelea kushuhudiwa katika chama tawala nchini Burundi cha CNDD-FDD, chama ambacho hapo awali kilileta matumaini ya kuwau...