Pages

lundi 24 février 2014

RAIS WA UGANDA YOWERI MUSEVENI ASAINI SHERIA TATA INAYO WABANA WATU WANAOJIHUSISHA NA NDOA ZA JINSI MOJA

Rais wa Uganda Yoweri Kaguta Museveni amesaini muswada tata unaopinga ndoa za watu wa jinsi moja, licha ya vitisho kutoka kwa mataifa ya Magharibi na Marekani kusitisha msaada na nchi hiyo iwapo atafikia hatuwa hiyo ya kusaini muswada huwa na kuwa sheria.

Akizungumza na waandishi wa habari muda mfupi baada ya kusani Muswada huo, rais Museveni amesema wanaojihusisha na vitendo hivyo ni wagonjwa, kwanini wasivutiwe na wanawake warembo waliopo, au wanaume ma handsame?

Muswada huo wa sheria uliyoidhinishwa katikati mwa mwezi wa desemba, unapinga mapenzi ya watu wa jinsi moja, na kuwalazimu watu kunyooshea kidole yeyote anaejihusisha na kitendo hicho.

Muswada huo ambao sasa utakuwa sheria, unatoa adhabu ya kifungo cha miaka 14 jela kwa wale watakaopatikana na hatia kwa mara ya kwanza.

Vifungo vya sheria vilivyozua utata, ambavyo vinatoa adhabu ya kifo kwa watu watakaorudi kushiriki kitendo cha watu wa jinsia moja, au mtu yeyote ambaye atapatikana ameshiriki kitendo hicho na mtoto wa kiume alie na umri ulio chini ya miaka 18, au anajitambua kwamba ameathirika na ukimwi, vifungo hivyo vilifutwa, lakini sheria hio bado inaendelea kukosolewa na wanaharakati wa haki za binadamu na mataifa ya magharibi.

Aucun commentaire:

Enregistrer un commentaire

KINACHOFANYWA NA RAIS NKURUNZIZA KWA SASA NDIO ULE MCHEZO WA NDANI?

Mkanganyiko umeendelea kushuhudiwa katika chama tawala nchini Burundi cha CNDD-FDD, chama ambacho hapo awali kilileta matumaini ya kuwau...