Wizara
ya mambo ya ndani nchini Ukraine imetangaza hati ya kukamatwa kwa
aliekua rais wa nchi hiyo Viktor Ianoukovitch, siku mili tu, baada
ya bunge kupiga kura ya kumuondoa madarakani kutokana na maandamano
yaliyosababisha mamia ya raia kupoteza maisha.
Mgawanyiko
umejitokeza nchini Ukraine baina ya wananchi baada ya rais Ianukovich
kuondoka madarakani ambapo upande mmoja wanaunga mkono taiufa hilo
kushirikiana na Umoja wa Ulaya na upande mwingine ukiounga mkono
ushirikiano na urusi.
Hayo
yanajiri wakati serikali ya Urusi ikikataa uhalali wa kiongozi wa
sasa wa taifa hilo, wakati huu serikali ikitowa wito wa kukamatwa kwa
aliyekuwa rais wa taifa hilo Victor Ianukovich na kuomba msada kwa
mataifa ya fedha kwa mataifa ya magharibi.
Umoja
wa Ulaya umeweka kando uwezekano wa kusaini mkataba na serikali mpya
ambayo inaanda uchaguzi kabla ya wakati Mei 25, na kukumbusha kuwa
msaada wowote wa kifedha utatolwa kwa masharti ya kufanyika
mabadiliko ya kiuchumi.
Wakati
huo huo mataifa jirani na Ukraine yametowa wito wa mazungumzo ya
wananchi wa taifa hilo ili kumaliza tofauti zao, siku moja baada ya
kuteiuliwa kwa uongozi mpya, huku mataifa hayo yakitowa wito wa
kuitolea msaada wa kifedha Ukraine.
Aucun commentaire:
Enregistrer un commentaire