Serikali
ya Marekani imesema inapitia upya mkataba wa ushirikiano wake na
serikali ya Uganda baada ya juma hili rais wa taifa hilo kupasisha
sheria inayo wabana wanandoa wa jinsi moja licha ya rais Obama
kumshinikiza kutofanya hivo.
Msemaji
wa Ikulu ya Marekani Jennifer Psaki amessma Marekani ni moja kati ya
wafadhili wakubwa wa serikali ya Uganda ambapo mwaka huu wa 2014
Uganda ilipokea msaada wa kitita cha dola milioni 485 ambazo kwa
silimia kubwa husaidia katika sekta ya Afya.
Waziri
wa mambo ya nje wa Marekani John Kerry amesema wanachokifanya kwa
sasa ni kupitia upya mahusiano yao na Uganda ambayo sasa inaonekana
kuwa kinara wa kuwanyima haki watu wanajinsia moja.
Wachambuzi
wa siasa wanaonakuwa serikali ya Uganda ilikuwa inatarajia kuwa hilo
litaftokea bila shaka wamejipanga kuziba hilo pengo.
Aucun commentaire:
Enregistrer un commentaire