Rais
wa Marekani, Barack Obama, baadae hii leo anatarajiwa kuwa na
mazungumzo na kiongozi wa kidini wa Tibeti, Dalai Lama anayeishi
uhamishoni, mazungumzo ambayo yamepingwa vikali na utawala wa China.
Utawala
wa Beijing uliiandikia barua ikulu ya Washington na kuitaka isitishe
mpango wa rais Obama kuwa na mazungumzo na kiongozi huyo ambaye China
inamtuhumu kama mhaini.
China
inasema iwapo rais Obama atafanya mkutano na Dalai Lama hakika
kutaathiri kwa sehemu kubwa uhusiano kati ya nchi hizo mbili.
Mara
ya mwisho rais Obama alikutana na Dalai Lama mwaka 2011 hatua ambayo
pia ilipingwa vikali na utawala wa Beijing.
Aucun commentaire:
Enregistrer un commentaire