Pages

mardi 18 février 2014

WAJUMBE WA BUNGE LA KATIBA NCHINI TANZANIA KUKUTANA LEO KWA MARA YA KWANZA JIJINI DODOMA


Kikao cha kwanza cha Bunge Maalumu la Katiba kinaanza leo mchana mjini Dodoma nchini Tanzania ambapo wajumbe zaidi ya Mia sita watakuwa na kazi ya kuandaa kanuni na taratibu ambazo zitatumika katika kumchagua mwenyekiti wa kudumu wa Bunge hilo.


Kikao hiki cha kwanzo kitaongozwa na Katibu wa Bunge la Jamhuri ya Muungano, Dk Thomas Kashililah na Katibu wa Baraza la Wawakilishi, Yahya Khamis Hamad, kazi kubwa itakayofanywa leo ni wajumbe wa Bunge hilo kupewa miongozo.


Kikao hicho kitaanza kwa kumchagua mwenyekiti wa muda miongoni mwa wajumbe 629 wa Bunge hilo na kazi yake kubwa itakuwa ni kuandaa kanuni na taratibu ambazo zitatumika katika kumchagua mwenyekiti wa kudumu wa Bunge hilo na kuanzisha mchakato wa vikao vyake.

Wito umekuwa ukitolewa kwa wajumbe hao kuweka maslahi ya wananchi na taifa mbele badala ya kuweka mbele msalahi yao binafsi na kuiboresha rasimu hiyo.

Hii ni hatua muhimu kwa wananchi wa Tanzania kuendelea kupata katiba mpya na hatma ya rasimu hiyo itabainika baada ya siku 70 ya wajumbe hao kuijadili na kuipitisha na baadaye raia wa Tanzania kuipigia kura ya maoni kuikubali au kuikataa.







Aucun commentaire:

Enregistrer un commentaire

KINACHOFANYWA NA RAIS NKURUNZIZA KWA SASA NDIO ULE MCHEZO WA NDANI?

Mkanganyiko umeendelea kushuhudiwa katika chama tawala nchini Burundi cha CNDD-FDD, chama ambacho hapo awali kilileta matumaini ya kuwau...