Rais wa Afghanistan Hamid Karzai ameinyoshea kidole marekani na kusema kuwa haipaswi kuingilia mambo ya ndani ya nchi yake kwa kuwa ina mamlaka kamili.
Haya yamekuja baada ya Marekani
kueleza kuchukizwa kwake na hatua iliyochukuliwa na mahakama nchini
Afganstan kuwaachia huru wafungwa 65 wa kundi la Taliban hatua ambayo
inavuruga uhusiano baina ya nchi hizo mbili.
Marekani
imesema kuwa wafungwa hao hawakupaswa kuachiwa kwa sababu wanahusika
na mauaji ya wanajeshi wa umoja wa kujihami wa nchi za magharibi,
NATO na wanajeshi wa Afghanstan.
Aucun commentaire:
Enregistrer un commentaire