Rais wa zamani wa Senegal Abdoulaye Wade anasubiriwa jijini Dakar hapo kesho April 23. Wade aliondoka nchini Senegal baada ya kuanguka kqwenye uchaguzi mkuu wa rais wa mwaka 2012. kurejea kwa Abdoulaye wade aliye tawala kuanzia mwaka 2000 hadi 2012, kumeahirishwa mara kadhaa lakini sasa imethibitishwa kuwa kesho anarejea nchini mwake, viongozi wa chama chake cha PDS wamethibitisha.
Abdoulaye
Wade mwenye umri wa miaka 87 aliongoza Senegal kwa kipindi cha miaka
kumi na miwili kabla ya kuanguka kwenye uchaguzi mkuu wa rais wa
March 25 mwaka 2012 dhidi ya mpinzani wake Macky Sall ambaye alikuwa
waziri wake mkuu kabla ya kuwa mpinzani.
Aliondoka
jijini Dakar Julay mwaka 2012 na kuelekea kueshi jijini Versaille
nchini Ufaransa pamoja na mkewe, na tangu hapo alikuwa bado hajarejea
nchini mwake, lakini amekuwa akihudhuria katika vikao mbalimbali
barani afrika na warabuni.
Aucun commentaire:
Enregistrer un commentaire