Kiongozi
wa kanisa katoliki duniani Papa Francis katika ujumbe wake wa siku ya
Pasaka, ameomba juhudi za kuwaunganisha watu waliohitilafiana zipewe
kipao mbele hususan nchini Syria, jamhuri ya Afrika ya kati, Sudani
Kusini na Venezuela na kusisitiza kuhusu unyonyaji, na kuwatupilia
watu lakini pia kuhusu umasikini ambo umekithiri kwa kiasi kikubwa
duniani.
Akihutubia
mbele ya watu wanaokadiriwa kufikia laki moja na nusu mbali na wale
waliokuwa wakifuatilia ibada hiyo ya misaa kupitia luninga mbalimbali
, Papa Francis amefahisha kwamba siku kuu ya pasaka mwaka huu
imesherehekewa tarehe moja na waumini wa kanisa la Arthodox.
Katika
maombi yake Papa Francis amemuomba mwenyezi Mungu alainishe nyoyo za
watu wanaohasiamiana katika mataifa ya Ukraine, Syria, Sudani Kusini,
jamhuri ya Afrika ya kati na venezuela kukubaliana swala la ujenzi wa
mataifa yao na kustaawisha amani.
Aucun commentaire:
Enregistrer un commentaire