Bunge la
Jumuiya ya Afrika Mashariki limelazimika kusitisha vikao vyake kwa
muda usiojulikana kufuatia kuibuka kwa malumbano ya kisheria katiu ya
wabunge kuhusu njia sahihi za kumuondoa spika wa bunge hilo dr
Magreth Zziwa.
Spika Zziwa
mwenyewe ndiye aliyetangaza kuahirisha kikao hicho kwa kutumia kanuni
za bunge hilo hatua aliyoifikia baada ya wabunge zaidi ya watano
kusimama wakitaka suala lake lijadiliwe ndani ya bunge huku wengine
wakipinga wakidai suala hilo liko mahakamani.
Spika Zziwa
na baadhi ya wabunge wanaomuunga mkono waliwasilisha kesi kwenye
mahakama ya Afrika Mashariki wakitaka ufafanuzi wa kisheria kuhusu
hatua zinazoweza kuchukuliwa ili kuleta bungeni hoja ya kumng'oa
spika.
Bunge hilo
lilitarajiwa kumaliza vikao vyake tarehe 4 ya mwezi April mwaka huu,
lakini kufuatia hatua ya kuahirishwa kwa vikao vyake sasa haijulikana
lini litarejea kwenye vikao vyake.
Aucun commentaire:
Enregistrer un commentaire