Pages

mardi 29 avril 2014

RAIS WA KENYA ASAINI SHERIATATA INAYORUHUSU NDOA ZAIDI YA MOJA







Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta amesaini jumanne hii sheria tata inayoruhusu ndoa zaidi ya moja bila hata kupata idhini ya mke wa kwanza.

Kwa mujibu wa taarifa ya kutoka Ilkulu ya rais nchini Kenya, sheria hiyo ilipasishwa bungeni mwezi March iliopita ambapo wabunge waliodowa kizuizi au kipengamizi kwa mke wa kwanza kupinga mumewe kuwa na mke zaidi ya mmoja, kitendo ambacho kiliwafanya wabunge wanawake bungeni kupatwa na hasira na kuondoka bungeni wakati sheria hiyo ikipigiwa kura.


Kwa mujibu wa sheria hiyo ya Kenya, ndo ni muungano huru kati ya ya mwanaume na mwanamke na inwezakuwa ya mke mmoja au zaidi ya mmoja na inaweza kufanyika katika hatuwa tofauti za kijadi.

Hata hivyo sheria hiyo hairuhusu mwanamume kuwa na mume zaidi ya mmoja.

Muungano wa makanisa nchini Kenya NCCK unaozikutanisha kanisa zaidi ya 40, umepigan vikali sheria hiyo, huku shirikisho la mawakili wanawake likiahidi kuwasilisha kesi mahakamani.


Hata hivyo shirikisho la kimataifa la haki za binadamu pamoja na tume ya haki za binadamu nchini Kenya licha ya kukosoa sheria hiyo ambayo haikuweka kikomo kwa idadi ya ndoa, wamepongeza hatuwa hiyo iliofikwa kwakuwa inalazimisha ndoa zote kuorodheshwa na hivo kuwa kama kinga kwa wanawake

Aucun commentaire:

Enregistrer un commentaire

KINACHOFANYWA NA RAIS NKURUNZIZA KWA SASA NDIO ULE MCHEZO WA NDANI?

Mkanganyiko umeendelea kushuhudiwa katika chama tawala nchini Burundi cha CNDD-FDD, chama ambacho hapo awali kilileta matumaini ya kuwau...