Serikali
ya Mrekani ambayo iliochangia kwa kiasi kikubwa kupatikana kwa taifa
la Sudani Kusni imetangaza kuwa itawachukulia vikwazo viongozi wa
taifa hilo changa pamoja na viongozi wa waasi ambao wanashindwa
kufikia muafaka wa kumaliza machafuko.
Rais
wa Barack Obama aliamuru tangu mwanzoni mwa mwezi huu utawala wake
kuwawekea vikwazo vya kuzuia mali za na kuwanyima viza za usafiri
viongozi wote wanaohatarisha juhudi za kusaka amani nchini Sudani
Kusini na kushambulia taasisi za umoja wa Mataifa pamoja na uvunjifu
wa haki za binadamu.
Vikwazo
hivyo vinawalenga wale wote wanaochochea machafuko kwa kuchafuwa
mchakato wa demokrasia na taasisi za serikali pamoja na kuvuruga
mchakato wa kutafuta amani, lakini pia kwa wale wanaovunja haki za
binadamu.
Aucun commentaire:
Enregistrer un commentaire