Rais
wa Marekani Barack Obama ameituhumu Urusi kwa kutoheshimu makubaliano
yaliofikiwa hivi karibuni jijini Geneva Uswisi kwa ajili ya
kuutafutia suluhu mzozo wa Ukraine.
Tuhuma
hizi za Obama zinakuja baada ya serikali ya Urusi kusema ipo tayari
kuingilia kati mzozo wa Mshariki mwa Ukraine iwapo faida zake
zitawekwa hatarini, hatuwa ambayo inakuja baada ya srikali ya Kiev
kutangaza kuanzisha operesheni dhidi ya wanaharakati wanaodai
mjitengo wa eneo hilo.
Kauli
hii ya Urusi inakuja kuhatarisha zaidi hali iliopo wakati huu jumuiya
ya kimataifa ikijaribu kulitafutia suluhu ya kudumu swala hilo.
Hali
ya matumaini ilishuhudiwa baada ya kufikiwa makubaliano ya kimataifa
jijini Geneva Uswisi, na sasa mvutano unaibuka upya kati ya Urusi na
mataifa ya magharibi.
Waziri
wa mambo ya nje wa Urusi Sergei Lavrov amesema iwapo faida zao
zitashambuliwa kama ilivyokuwa katika eneo la Ossetie, haoni njia
nyingine mbali na kujibu kwa kutumia sheria za kimataifa.
Aucun commentaire:
Enregistrer un commentaire