Pages

mercredi 9 avril 2014

TUME HURU YA UCHAGUZI NCHINI BURUNDI CENI YAVITAKA VYAMA VYA KISIASA VILIVYO GAWANYIKA KUUNGANA KABLA YA UCHAGUZI MKUU WA 2015


Mwenyekiti wa tume huru ya uchaguzi nchini Burundi CENI Pierre Claver Ndayicariye amevitaka vyama vilivyo gawanyika kutokana na sababu mbalimbali, kuhakikisha vimeungana kabla ya uchaguzi mkuu wa mwaka 2015. Hatuwa hiyo amesema itaongeza chachu ya kukuwa kwa Demokrasia nchini Burundi.

Pierre Claver Ndayicariye amesema wakati utashi baina ya viongozi wa kisiasa na wafuasi wa vyama hivyo unadhihirika wazi, haifai kuipa nafasi mtengano wa kisiasa, na kuendelea kuwa CENI inataka mchakato wa kisiasa utaoshirikisha vyama vilivyoungana.

Mbali na hilo Ndayicariye amesema katika uchaguzi ujao wa mwaka 2015, kadi ya uraia inayo tumiwa kwa sasa(Karangamuntu) ndiyo itayopewa nafasi katika uchaguzi huo na sio ambayo ipo mbioni kutumiwa na ambayo shughuli za kujiorodhesha zinasimamiwa na wizara ya mambo ya ndani.

Kiongozi huyo wa tume huru ya Uchaguzi nchini Burundi CENI Amesema wakati wa shughuli za kujiorodhesha kwenye daftari la wapiga kura, kadi hiyo mpya(Biometrique) itakuwa haijawa tayari, hivo kadi inayotumika sasa ndio ambayo itayopewa nafasi.

Aucun commentaire:

Enregistrer un commentaire

KINACHOFANYWA NA RAIS NKURUNZIZA KWA SASA NDIO ULE MCHEZO WA NDANI?

Mkanganyiko umeendelea kushuhudiwa katika chama tawala nchini Burundi cha CNDD-FDD, chama ambacho hapo awali kilileta matumaini ya kuwau...