Rais wa Rwanda Paul Kagame, amekuwa akiongoza mikutano katika vyuo mbalimbali nchini Marekani wakati huu wa maadhimisho ya kumbukumbu ya miaka 20 ya mauaji ya kimbari nchini Rwanda. akizungumza katika chuo kikuu cha Tuft cha Massachussetts ,rais Kagame ameulizwa kuhusu mustakabali wake wa kisiasa wakati huu muhula wake wa pili na wa mwisho ukielekea tamati kulingana na katiba ya Rwanda.
Serikali ya Washington inaomba uwepo wa uhuru wa kutowa maoni baada ya kutiwa nguvuni kwa watu kadhaa jijini Kigali hususan msanii Kizito Mihigo.
Akiulizwa iwapo Paul Kagame atawania uchaguzi au la mwaka 2017 na kubadili katiba? Rais Kagame amesema wananchi ndio wataoamuwa, kwa sasa inafaa kuiacha nchi na wananchi wake kujuwa nini wanataka, na hii ndio hatuwa kubwa muhimu. Kagame amesema tangu yupo madarakani amekuwa akiulizwa iwapo ataondoka madarakani, amesema yupo kwa ajili ya kusimamia maswala muhimu ya wananchi, wanyarwanda ndio waamuzi.
Upande wake mpinzani mkuu wa Rwanda Faustin Twagiramungu aishie uhamishoni nchini Ubelgiji amesema unapoulizwa swali unatakiwa kujibu ndio au hapana, lakini ukisema wananchi, unamaanisha kura ya maoni na kura ya maoni ni nini, hii inamaanisha katiba itabadilishwa. Amemalizia kuwa watu wanatakiw akujuwa kwamba hakuna upana wa kisiasa.
Aucun commentaire:
Enregistrer un commentaire