Pages

jeudi 24 avril 2014

INTAMBA MU RUGAMBA KUWASILI JIONI HII JIJINI DAR ES SALAAM KUMENYANA NA TAIFA STARS

Vijana wa timu ya taifa ya Burundi Intamba Mu Rugamba, wanasubiriwa leo jijini Dar Es Salaam kwa ajili ya mechi ya kirafiki na Tifa Stars itayopigwa April 26 kwenye Uwanja wa taifa jijini Dar es Salaam.

Didier Kavumbagu mshambuliaji anaekipiga katika Klabu ya Yanga pamoja na mshindi wa mabao katika ligi kuu ya Vodacom msimu uliopita Amisi Tambwe anaepiga soka ya kulipwa katika klabu ya Wekundu wa Msimbazi Simba, watajiunga na wenzao kwa ajili ya mechi hiyo.

Vijana wa Intamba Mu Rugamba watasimamiwa na makocha wasaidizi Niyungeko Olivier Mutombola pamoja na Ndayizeye Jimmy baada ya kocha mkuu Muholanzi Rainer Wilfried kuwa safarini.

Vijana wa Taifa Stars upande wao wamejiandaa vizuri kuwakabili ndugu zao Warudi.

Na hii ndio orodha ya wachezaji wa Intamba Mu Rugamba wataosuguana na Taifa Stars ya Tanzania:

1. ARAKAZA Mc ARTHUR / Flambeau de l'Est
2. BIHA Omar / Vital'o Fc
3. KIZA Fataki / LLB
4. RUGONUMUGABO Stéphane/LLB
5. HAKIZIMANA Issa / LLB
6. HARERIMANA Rashid /LLB
7. NDIKUMANA Yussuf Lule / LLB
8. MOUSSA Mossi / Vital'o Fc
9. NAHIMANA Shassir / Inter star
10. NDARUSANZE Claude / LLB
11. NZIGAMASABO Steve /Vital'o fc
12. SHABANI Hussein Tsabalala / Flambeau de l'Est
13. NKURIKIYE Léopold / Inter star
14. HAKIZIMANA Pascal / Flambeau de l'Est
15. Amissi Cédric / Rayon sport
16. Jumapili Idon / Vital'o Fc
17. Amissi Tambwe / Simba Sc
18. KAVUMBAGU Didier / Yanga Africans.

Aucun commentaire:

Enregistrer un commentaire

KINACHOFANYWA NA RAIS NKURUNZIZA KWA SASA NDIO ULE MCHEZO WA NDANI?

Mkanganyiko umeendelea kushuhudiwa katika chama tawala nchini Burundi cha CNDD-FDD, chama ambacho hapo awali kilileta matumaini ya kuwau...