Cheikh Abubakar Shariff Ahmed wakati wa uhai wake |
Polisi
kwenye mji wa Mombasa hii leo wameendelea kuimarisha usalama kwenye
mji wa Mombasa kufuatia kuuawa kwa kiongozi wa dini ya kiislamu jana
usiku na watu wasiojulikana, tukio ambalo limewashtua wengi.
Sheikh
Abubakar Shariff Ahmed alikuwa ni moja kati ya viongozi waliokuwa
wakimuunga mkono Osama Bin Laden na alikuwa kwenye orodha ya vikwazo
vya Umoja wa Mataifa UN kwa tuhuma za kuwa mstari wa mbele kutoa
msaada na mafunzo kwa vijana wa Kenya kujiunga na kundi la Al-Shabab
nchini Somalia.
Hali ya
utulivu iliripotiwa kwenye maeneo mengi ya mji wa Mombasa wakati huu
kukiwa na hofu ya kiusalama hasa kwa vijana ambao walikuwa wafuasi wa
karibu wa Sheikh Ahmed aliyefahamika pia kwa jina la Makuburi.
Kumeibuka
maswali kuhusu ni nani hasa aliyehusika na kifo cha kiongozi huyu na
kama ni muendelezo wa mauaji ya viongozi wa kidini waliomstari wa
mbele kuunga mkono sera za Al-Shabab na Al-Qaeda nchini Kenya?
Aucun commentaire:
Enregistrer un commentaire