Rais wa Burundi Pierre Nkurunziza
amekutana na wawakilishi wa kundi la vijana wa chama tawala CNDD-FDD
Imbonerakure kutoka katika mikoa yote ya Burundi. Mkutano huo
umefanyika siju ya Jumamosi ya juma lililopita katika Mkoa wa Ngozi.
Mkutano huu unakuja siku kadhaa baada ya kuwepo kwa taarifa za ugavi wa silaha kwa vijana hao wa chama tawala, taarifa iliozua msuguano baina ya Utawala wa Bujumbura na Umoja wa Mataifa
Kila Mkoa umewakilishwa na vijana 3
akiwepo pia mwenyekiti wa chama hicho Pascal Nyabenda. Watafiti wa
mambo wanaonakuwa kikao hicho kitaza matunda kwani vijana kutoka
chama hicho wanaweza kubadili mwenendo wao hasa katika kueshi na
wengine kwa hali ya kawaida.
Baada ya kikao hicho mwenyekiti wa
chama Cndd-Fdd, amewaambia waandishi wa habari kwamba kikao hicho
kilikuwa katika ajenda ya program za chama hicho, lakini kwa vile
kuna swala linazungumziwa kuhusu vijana, hivyo washiriki
wamezungumzia kwa kina na kubadilishana kuhusu yanayojiri.
Aucun commentaire:
Enregistrer un commentaire