Umoja
wa Mataifa UN umesema unafanya kila jitihada kuzuia mauaji ya kimbari
yalioshuhudiwa nchini Rwanda yasitokei nchini Sudani Kusini. Viongozi
wa Umoja huo wametaarifu viongozi wa serikali ya Sudani Kusini na
waasi wanaomtii Riek Machar makam wa rais zamani kuwa ndio
wataoulizwa iwapo mauaji hayo yatatokea.
Mkuu
wa tume ya haki za bindamau kwenye Umoja wa Mataifa Navy Pillay
ambaye amezuru nchini Sudani Kusini wiki hii amesema hali iliopo
nchini Sudani Kusini inatisha, na kuna kila dalili za kutokea kwa
machafuko makubwa ambapo viongozi wa nchi hiyo na Jumuiya ya
kimataifa hawaoni uzito wa hali iliopo.
mapigano
kati ya majeshi ya serikali na waasi, wa Riek Machar yameanza
kushuhudiwa tangu mwezi desemba mwaka jana na ambayo yamefuatiwa na
mauaji yaneye misingi ya kikabila kati ya watu wa kabila la rais
Salva Kiir la Dinka na lile na Nuer la Riek Machar
Navy
Pillay ambaye amfanya ziara ya siku mbili nchini Sudani Kusini
amesema machafuko ya hivi karibuni katika mji wa Bentui ambapo watu
zaidi ya mia moja walipoteza maisha, ni kiashiria tosha cha hali
mbaya ilipo nchini humo.
Aucun commentaire:
Enregistrer un commentaire