Kumeripotiwa
maandamano makubwa mjini Brussels Ubelgiji hapo jana na leo asubuhi,
maandamano yanayodaiwa kufanywa na raia wa Burundi wanaoishi barani
Ulaya wakipinga hatua ya Serikali yao kutaka kufanyia mabadiliko
katiba ya nchi na rais Kuongezewa muhula mwingine wa tatu. Jambo ambalo wanasema ni kinyume cha sheria ya nchi hiyo.
Maandamano hayo ya jijini Brussels yanakuja baada ya yale yaliotokea huko Marekani mwishono mwa Juma lililopita na katika maeneo mengine barani Ulaya
Mbali na
kupinga kufanyika kwa mabadiliko yoyote ya katiba ya nchi, raia hao
wanataka serikali iheshimu uhuru wa vyombo vya habari pamoja na
kutominya uhuru wa vyama vya upinzani kufanya siasa za wazi
zinazokosoa mwenendo wa Serikali.
Maandamano
haya yanafanyika wakati huu ambapo nchi ya burundi inashuhudia
mabadiliko makubwa ya kisiasa na kiutawala ambapo baadhi ya viongozi
wa upinzani wamejikuta wakiwekwa kizuizini na Serikali kwa tuhuma za
kutaka kuchochea vurugu nchini humo hatua ambayo hata Umoja wa
Mataifa umeonya kuendelea kushuhudiwa kwa hali hiyo.
Aucun commentaire:
Enregistrer un commentaire