Kwa
mara ya kwanza toka uteuzi wake mwaka uliopita, kiongozi wa kanisa
katoliki duniani Papa Francis hii leo ameomba radhi hadharani
kufuatia kashfa ya kulawiti watoto dhidi ya mapadri na maaskofu wa
kanisa hilo.
Akizungumza
na kituo cha redio cha kanisa mjini Vatican, Papa Francis ameomba
radhi kwa niaba ya kanisa kwa familia na watoto waliofanyiwa vitendo
vya udhalilishaji.
Papa
Francis amekiri kanisa lake kufahamu matukio ya watoto kudhalilishwa
na kwamba wanarekebisha makosa yaliyojitokeza na kuahidi
kuwashughulikia kidini viongozi wote waliohusishwa kwenye tuhuma ya
kulawiti watoto wadogo.
Hivi
karibuni kanisa hilo lilijikuta kwenye shinikizo kubwa baada ya
ripoti ya haki za binadamu ya Umoja wa Mataifa kulaani vitendo hivyo
na kulitaja moja kwa moja kanisa katoliki kwa kuwafumbia macho
mapadri waliohusika na vitendo hivi.
Aucun commentaire:
Enregistrer un commentaire