Pages

mercredi 30 avril 2014

VIONGOZI WA JUMUIYA YA AFRIKA MASHARIKI WAMEKUTANA JUMATANO HII JIJINI ARUSHA

Ma rais Jakaya Kikwete kushoto, Uhuru kenyatta kati, na Yoweri museveni kulia
Mwenyekiti wa Jumuiya ya Afrika Mashariki ambaye pia ni rais wa Kenya Uhuru Kenyatta ametoa wito kwa nchi wanachama kutekeleza maazimio yaliyokubaliwa katika miaka iliyopita ili kuimarisha Jumuiya hiyo.

Akizungumza katika Mkutano wa viongozi wa Jumuiya hiyo mjini Arusha Tanzania makao makuu ya Jumuiya hiyo, rais Kenyatta amesisitiza kuwa makubaliano yaliofikiwa ya matumzi ya sarafu moja mwaka uliopita ni mwanzo wa mafanikio ya Jumuiya hiyo na wananchi wa mataifa hayo kutengamana kwa urahisi

Kuhusu mzozo wa Sudan Kusini, rais Kenyatta amesema kuwa Jumuiya hiyo itafanya kila kilicho ndani ya uwezo wake kusaidia kurejesha amani lakini akatoa wito kwa pande mbili zinazozazana kuacha vita na kukubaliana.

Mazungumzo ya kujadili ombi la Sudan Kusini kujiunga kama Mwanachama wa Jumuiya hiyo yameahirishwa hadi mwezi Septemba mwaka huu. Mbali na rais Kenyatta viongozi wengine waliohudhuria mkutano huo ni pamoja na rais wa Tanzania Jakaya Kikwete, rais Uganda Yoweri Museveni, Makamu wa rais wa Burundi Prosper Bazombanza na Waziri Mkuu wa Rwanda Pierre Damien Habumuremyi.

Aucun commentaire:

Enregistrer un commentaire

KINACHOFANYWA NA RAIS NKURUNZIZA KWA SASA NDIO ULE MCHEZO WA NDANI?

Mkanganyiko umeendelea kushuhudiwa katika chama tawala nchini Burundi cha CNDD-FDD, chama ambacho hapo awali kilileta matumaini ya kuwau...