Baada
ya majuma kadhaa ya tuhuma mbalimbali za rushwa na matumizi mabaya ya
fedha, Serikali ya Kenya imetangaza mikakati mipya ya ubanaji
matumizi, ambapo imepiga marufuku safari na mafunzo yasiyo ya lazima
kwa wafanyakazi wa umma.
Waziri
wa fedha Henry Rotich amesema kuwa tayari ameshatoa waraka kwa
maofisa wa wizara na vitengo mbalimbali vya uma, akipiga marufuku
safari za nje na matumizi mengine yasiyo ya lazima.
Waziri
Rotich amesema safari za mafunzo za ndani na zile za kaunti zimepigwa
marufuku.
Hatua
hii itasaidia Serikali ya Kenya kupunguza matumizi makubwa
yanayolalamikiwa na upinzani pamoja na wananchi? Mwenzangu Victor
Abuso amezungumza na James Shikwati mchambuzi wa masuala ya Uchumi
akiwa jijini Mwanza nchini Tanzania.
Aucun commentaire:
Enregistrer un commentaire