Taarifa za hivi punde zinaeleza kwamba washambuliaji wawili waliokuwa miongoni mwa watu waliosambulia na kuwateka watu katika Hoteli moja jijini Bamakao wameuawa wakati wa operesheni za uokozi.
Hayo yanajir wakati huu Wizara ya mambo ya ndani nchini Ufaransa, imethibitisha kupelekwa kwa kikosi maalumu cha wanajeshi wa kukabiliana na ugaidi na hali ya hatari nchini Mali, ambako wanamgambo wenye silaha wanashikilia mateka wat zaidi ya 150 kwenye hoteli moja mjini Bamako.
Zaidi
ya wanajeshi 40 wa kikosi maalumu cha Ufaransa cha GIGN wanaelekea
nchini Mali kutoa msaada kwa vikosi vya Mali kujaribu kuwaokoa mateka
wanaoshikiliwa kwenye hoteli ya Radisson Blu, hoteli inayowahifadhi
wageni na maofisa kadhaa wa Umoja wa Mataifa.
Hatua
hii ya Ufaransa imekuja ikiwa ni saa chache tu zimepita toka
wapiganaji wenye silaha kuvamia hoteli hiyo na kuwashikilia mateka
wageni waliofikia kwenye hoteli hiyo.
Aucun commentaire:
Enregistrer un commentaire